Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
WAGONJWA WASHAURIWA KUTUMIA MAZIWA SAFI NA SALAMA ILI KUTUNZA AFYA ZAO
20 Jun, 2023
WAGONJWA WASHAURIWA KUTUMIA MAZIWA SAFI NA SALAMA ILI KUTUNZA AFYA ZAO

KATIKA kukabiliana na tatizo la utapia mlo, Bodi ya Maziwa Tanzania imegawa maziwa kwa wagonjwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kujenga afya njema kwa wagonjwa  pamoja na kuwahamasisha  kutumia maziwa ili waweze kuimarisha afya zao na lishe bora.

 Mtekinolojia wa Chakula kutoka Bodi ya Maziwa Tanzania Bi. Neema Moshi amesema wagonjwa wanatakiwa kunywa maziwa wanapokula chakula na baada ya kumeza dawa maana maziwa ni mlo kamili.

Amesema kuna aina mbili tu ya dawa ambazo mgonjwa haruhusiwi kunywa maziwa baada ya kumeza dawa hizo ambazo ni maginiziamu na dawa zenye mchanganyiko wa madini ya potashiamu kwani sio salama kiafya kwa mgonjwa tofauti na hapo dawa zingine ni salama na mgonjwa anaruhusiwa kutumia maziwa baada ya kula na kumeza dawa.

" Maziwa yanaongeza nguvu mwilini lakini pia maziwa yanaondoa msongo wa mawazo kwa mtumiaji kwani ni kiburudisho kwa mtu anaye  tumia maziwa lakini pia unaweza ukatengeneza juisi kwa kuchanganya ndizi mbivu na karoti hii inamsaidia mgonjwa kuongeza hamu ya kula,

" Tunashauri mtu anayesumbuliwa na vidonda vya tumbo kutumia maziwa glasi moja baada ya kula kwani maziwa yanapo ingia tumboni kabla ya kula chakula yanatengeneza utando ambao unapunguza maumivu na baada ya masaa mawili Asidi iliyoko tumboni (HYDROCLRIC ACID ) inapambana na Asidi iliyokokwenye maziwa ( LACTIC ACID ) na kumsababishia mgonjwa maumivu makali, tunataka tutoe dhana ya kwamba maziwa yanatibu vidonda vya tumbo " ameeleza Bi. Neema

Naye kaimu Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali yaRufaa ya Mkoa waDodoma Bi. Particia Kabendera amesema maziwa yanahitajika kwa kiasi kikubwa katika hospitali ya rufaa Dodoma kwa ajili ya watoto hasa wanaosumbuliwa na utapia mlo lakini pia kwa wagonjwa na watu wote kutumia maziwa kwani ni mlo kamili na bora kiafya.

" Tunaomba wadau wajitokeze ilikuwachangia watoto wanaosumbuliwa na utapia mlo wapate lishe bora ikiwemo maziwa kawa walivyofanya Bodi ya Maziwa Tanzania,

"Lakini pia tunatoa ushauri kwa watu wote watumie maziwa kwa wingi ili wajenge Kinga ya mwili tuwashukuru sana Bodi ya Maziwa Tanzania kwa kujitokeza kwa wagonjwa kuwapatia maziwa tunaamini wamefurahia na watatumia kwa afya zao" ameeleza Bi. Patricia

Vilevile Bi. Jenipher Mwali kwaniaba ya  wazazi  kutoka wodi ya watoto ametoapongezi kwa Bodi ya Maziwa Tanzania kwa kile ambacho wamekifanya na kuwataka watu wajitokeze na kutoa msaada itakayosaidia katika hospitali ya rufaa mkoa wa Dodoma. 

"Tunayo furaha kubwa kwa upendo mliotuonesha kutoka Bodi ya Maziwa tunaomba muendelee na moyo wa kujitolea zaidi na zaidi,

"Lakini pia wadau wengine pamoja na makampuni na taasisi mbalimbali nao wahamasike na kujitokeza ili kuweza kutusaidia na Mungu awabariki" ameeleza Bi. Jenipher

Pia, Afisa Ustawi wa Jamii hospitali ya rufaa mkoa wa Dodoma Bi.Tegemea Kulwa amesema wadau wazidi kujitokeza iliwaweze kuwasaidia watoto walio na utapia mlo wapate lishe bora pamoja na misaada mingine ya kijamii kama walivyofanya Bodi ya Maziwa Tanzania.

"Tunawashukuru Bodi ya Maziwa Tanzania kwa upendo wenu mliouonesha kwa wagonjwa tuombe tasisi mbalimbali wajitokeze ilikusaidia wagonjwa wapate lishe Bora ,

"Hospitali yetu bado inachangamoto kubwa ya maziwa safi na salama sio tu ya ng'ombe bali hata maziwa maalumu kwa ajili ya watoto wachanga na wale ambao wazazi hawana maziwa ya kutosha hivyo wadau wakijitokeza itasaidia kupunguza tatizo na kuimarisha afya zao" amesema Bi. Tegemea

Bodi ya Maziwa Tanzania imeungana na Taasisi nyingine za Serikali katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma hapa nchini kwa kuwatembelea wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma nakutoa elimu ya umuhimu wa kutumia maziwa pamoja na kugawa maziwa kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.