Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
TDB YAWASHIKA MKONO WASINDIKAJI WADOGO WA MAZIWA
09 Jun, 2023
TDB YAWASHIKA MKONO WASINDIKAJI WADOGO WA MAZIWA

Bodi ya Maziwa Tanzania imetoa msaada wa vifaa vya kubebea Maziwa (Kens) kwa makundi matatu ya wasindikaji wadogo wakati ikiadhimisha wiki ya Maziwa yaliyofanyika hivi karibuni mkoani Tabora.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa wasindikaji hao, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amewataka wanufaika wa vifaa hivyo kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ilikulinda ubora wa maziwa na kulinda afya ya mlaji.

"Maziwa yetu yanapoteza ubora Kwa sababu yanawekwa kwenye vyombo ambavyo havitakiwi kisheria, ninyi mmepewa vifaa hivi ilimtusaidie kuwaonesha wafanyabiashara wengine wa maziwa kuwa wanatakiwa kutumia vifaa bora vyakuhifadhia Maziwa Kama hivi, hivyo tunaamini mtakuwa mabalozi wema huko kwenye maeneo yenu" amesema Waziri Ulega

Pia Mheshimiwa Waziri ametumua fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara wote wanaojihusisha na biashara ya Maziwa kutumia vifaa bora vinavyopatikana hapa nchini hii itasaidia kurasimisha sekta ya Maziwa kwa haraka.

Bi. Nasinya mmoja wa wasindikaji wadogo waliopokea vifaa hivyo ameishukuru TDB Kwa namna inavyowasaidia na kuwainua wasindikaji wadogo kwakuwapa elimu ya kitaalamu ya namna bora ya usindikaji maziwa na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao.