Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
TAASISI ZA FEDHA ZASHIRIKI WIKI YA MAZIWA TABORA
09 Jun, 2023
TAASISI ZA FEDHA ZASHIRIKI WIKI YA MAZIWA TABORA

Taasisi zinazotoa huduma za fedha hapa nchini zimeshiriki maadhimisho ya Wiki ya Maziwa zilizofanyika kitaifa Mkoa wa Tabora kuanzia tarehe 29 Mei mpaka tarehe 01 Juni 2023 na kuyaongezea uzito maadhimisho hayo.

Katika maadhimisho hayo taasisi zilizoshiriki ni pamoja na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Benki ya NMB, SELF MICROFINANCE na UTT AMIS ambapo Kwa pamoja imetoa elimu ya kifedha Kwa wadau wa maziwa walioshiriki kwenye maadhimisho kwa kuwawezesha kuwapa mbinu mbalimbali za namna yakupata mitaji ya kuendeleza biashara zao pamoja na namna yakutunza kumbukumbu za kibiashara wanazofanya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau wa maziwa wamepongeza juhudi zilizofanywa na Bodi ya Maziwa Tanzania kwakushirikisha taasisi hizo za fedha kwani zimewapa upeo mpana wa namna yakufanya biashara kwa tija na kuwaunganisha kwenye taasisi hizo ili waweze kupata mikopo yenye riba nafuu.

Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa huwafanyika kila mwaka mwishoni mwa mwezi Mei na kufikia kilele chake tarehe 01 Juni ya kila mwaka ambapo kwa mwaka huu yamefanyika mkoani Tabora ikiwa na wadau zaidi ya 50 walioshiriki kuonesha bidhaa zao.