Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
MADIWANI MBULU DC WAIPA KONGOLE BODI YA MAZIWA
14 Jul, 2023
MADIWANI MBULU DC WAIPA KONGOLE BODI YA MAZIWA

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoa wa Manyara wameipongeza Bodi ya Maziwa Tanzania kwakuwaweka karibu wadau wa maziwa na kuwatafutia fursa za kujitangaza kimataifa kupitia majukwaa mbalimbali ya kibiashara.

Pongezi hizo zimetolewa na madiwani hao kupitia Kwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Joseph Mando walipotembelea banda la Bodi ya Maziwa Tanzania katika maonesho ya 47 ya kimataifa ya kibiashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

" Kwa niaba ya madiwani wenzangu tuliotembelea maonesho haya ya kibiashara nipende kuwapongeza sana Bodi ya Maziwa kwakuendelea kutimiza majukumu yenu yakuwaunganisha wadau wote walio katika mnyororo wa thamani kwenye Tasnia hii ya Maziwa.

"sisi Kama madiwani tumeona jinsi mnavyowajali wadau wenu kwakuwatafutia fursa Kama hizi zakuja kujitangaza kwenye maonesho Kama haya yanayowaleta watu wengi pamoja kwakufanya hivi kunasaidia wadau wa maziwa kuonekana ulimwenguni"  Amesema Mhe. Mando

Naye Diwani wa Viti maalumu wa Halmashauri hiyo Mhe. Ester Getagno ameshauri taasisi nyingine za serikali kuendelea kuwalea wadau wake wanaofanya shughuli zinazoitangaza taasisi husika ilikuendelea kuwakuza kiuchumi na kuendelea kuhudumia kundi kubwa zaidi la wananchi.

Vilevile Mtaalamu wa Mifugo Bw. Sifaeli Dalei toka kampuni ya Bajuta inayojishughulisha na uuzaji wa pembejeo za Mifugo hasa vifaa vya kukamulia na kuhifadhia Maziwa ameishukuru Bodi ya Maziwa kwakuipa nafasi yakushiriki katika maonesho hayo ya Kimataifa ya kibiashara kwani imewaongezea uwanja mpaka wa kibiashara Kwa wananchi waliokuwa wanatembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wadau hao.

 Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya kibiashara hufanyika kila mwaka kwakuwaleta wafanyabiashara wakubwa Kwa wadogo na wajasiriamali mbalimbali Kwa lengo la kiwakutanisha Kwa pamoja na kubadilishana uzoefu wa Biashara vilevile kujitangaza zaidi kitaifa na kimataifa.