Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
BUNGE YAANZA KUTEKELEZA MPANGO WA UNYWAJI MAZIWA SHULENI
26 Jul, 2023
BUNGE YAANZA KUTEKELEZA MPANGO WA UNYWAJI MAZIWA SHULENI

Baada ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah H. Ulega (MB) kuzindua Mpango kazi wa Unywaji Maziwa Shuleni wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa Mkoani Tabora Mei, 2023 Shule ya Msingi Bunge iliyopo Jijini Dar es Salaam hivi karibuni imeanza kutekeleza Mpango wa Unywaji Maziwa Shuleni unaoratibiwa na Bodi ya Maziwa Tanzania kwakushirikiana na Wasindikaji wa Maziwa hapa nchini ili wanafunzi kutumia maziwa yaliyosindikwa ambayo ni salama kwa afya zao.

Akizungumza shuleni hapo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge Mwl. Leonida Mulekuzi ameishukuru Bodi ya Maziwa Tanzania Kwa kuja na mpango wa Unywaji Maziwa shuleni kwani Maziwa yanafaida nyingi Kwa watoto hasa wanafunzi kwani uwepo wa programu hii itawasaidia wanafunzi ku tokuhangaika huko nje kutafuta vitu vya kula ambavyo havina umuhimu wowote katika ukuaji wao.

Naye Msimamizi wa mauzo wa kampuni ya Maziwa ya Tanga Fresh (LTD) Bw. Kephas Gembe ameushukuru uongozi wa shule ya Msingi Bunge Kwa namna walivyoupokea mpango huo kwakutoa ushirikiano wa Hali ya juu Hali iliyowezesha wanafunzi zaidi ya 1200 kunywa Maziwa Kwa siku moja idadi ambayo hakuna shule iliyoifikia Kwa siku moja.

'Naushukuru uongozi wa Shule ya Msingi Bunge kupitia kwa Mwalimu Mkuu kwakuanda utaratibu mzuri ambao utawawezesha wanafunzi kunywa maziwa mar moja kwa kila wiki ambapo kwa mwezi mmoja angalu kila mwanafunzi atakunywa maziwa mara nne' Amesema Bw. Gembe

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi wa shule hiyo wameonesha kufurahia sana mpango huo wa kunywa Maziwa shuleni kwani wamesema kwa mujibu wa wanavyofundishwa darasani Maziwa yanaupatia mwili virutubisho vingi ukilinganisha na vyakula vingine wanavyokula mtaani.

Bodi ya Maziwa Tanzania ndio taasisi pekee iliyopewa nguvu ya kisheria kusimamia, kuratibu na kuendeleza Tasnia ya Maziwa nchini ambapo katika kutekeleza majukumu hayo, Bodi ya Maziwa inahamasisha matumizi ya Maziwa na bidhaa zake pamoja ili kuimarisha afya za wanafunzi kupitia programu za Unywaji Maziwa Shuleni inayotekelezwa katika shule 134 hapa nchini.