Imewekwa: 06th December, 2018
Bodi ya Maziwa Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) wamesaini mkataba wa makubaliano (MoU) tarehe 30.11.2018 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwasaidia wadau wa sekta ya maziwa katika mnyoro wa thamani. Mkataba huo uliosainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa Bw. Lucas Malunde na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo, Mr Augistino Chacha umelenga kufanikisha mambo makuu 5;
- Kujenga uwezo wa wadau waliomo kwenye mnyororo wa thamani kupitia mafunzo
-Kuboresha upatikanaji wa pembejeo, mbari na malisho
-Kuboresha upatikanaji wa mikopo kwa wadau
-Kuboresha upatikanaji wa Teknolojia
-Kuongeza ufanisi katika mnyororo wa thamani