SIKU YA WANAWAKE DUNIANI "WEKEZA KWA WANAWAKE HARAKISHA MAENDELEO YA TAIFA NA USTAWI WA JAMII"
Pichani ni sehemu ya washiriki wa hafla ya kukabidhi Ng’ombe kwa Kampuni ya Kahama Fresh iliyofanyika katika shamba la Mifugo la Kampuni hiyo lililopo wilayani Karagwe, mkoani Kagera Januari 23, 2024.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na kikundi cha kina mama wanufaika wa programu ya Kopa Ngombe Lipa Maziwa muda mfupi baada ya kuzindua programu hiyo iliyofanyika kwenye shamba la Mifugo la Kampuni ya Kahama Fresh lililopo wilayani Karagwe, mkoani Kagera Januari 23, 2024.
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Prof. Goerge Msallya akitoa neno fupi kuhusu Tasnia ya Maziwa katika hafla ya kukabidhi Ng’ombe kwa Kampuni ya Kahama Fresh iliyofanyika katika shamba la Mifugo la Kampuni ya Kahama Fresh lililopo wilayani Karagwe, mkoani Kagera Januari 23, 2024.
Naibu Katibu Mkuu, Prof. Daniel Mushi akitoa neno la utangulizi katika hafla ya kukabidhi Ng’ombe kwa Kampuni ya Kahama Fresh iliyofanyika katika shamba la Mifugo la Kampuni ya Kahama Fresh lililopo wilayani Karagwe, mkoani Kagera Januari 23, 2024.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akikagua Ng’ombe ikiwa ni ishara ya kuwakabidhi kwa wanufaika wa programu ya Kopa Ngombe Lipa Maziwa katika hafla iliyofanyika kwenye shamba la Mifugo la Kampuni ya Kahama Fresh lililopo wilayani Karagwe, mkoani Kagera Januari 23, 2024.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na Wananchi (hawapo pichani) katika hafla ya kukabidhi Ng’ombe kwa Kampuni ya Kahama Fresh ambao watakopeshwa vijana na Wanawake waweze kujikwamua kiuchumi kupitia uzalishaji wa maziwa. Hafla hiyo imefanyika katika shamba la Mifugo la Kampuni ya Kahama Fresh lililopo wilayani Karagwe, mkoani Kagera Januari 23, 2024.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni Contractus, Bw. Witold Karczewski (wapili kulia) muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo yao kuhusu uwekezaji katika tasnia ya maziwa yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya waziri huyo jijini Dar es Salaam Januari 18, 2024. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu, Prof. Riziki Shemdoe. Wa kwanza kushoto ni Msajili wa Bodi ya Maziwa, Prof. George Msalya na wa kwanza kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara ya Poland ambaye pia ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Contractus, Bw. Adam Borawski.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Contractus, Bw. Witold Karczewski wakati wa mazungumzo yao kuhusu uwekezaji katika sekta ya maziwa yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya waziri huyo jijini Dar es Salaam Januari 18, 2024. Kulia kwake ni Katibu Mkuu, Prof. Riziki Shemdoe na kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara ya Poland ambaye pia ni Meneja Mauzo wa Kampuni, Bw. Adam Borawski.